January 12, 2019


Mwanachama wa Klabu ya Yanga na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amemvaa Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara kwa kumtaka aache siasa kuelekea katika mechi yao dhidi ya JS Saoura ya Algeria na badala yake asubirie dakika 90 ziamue.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani leo Jumamosi kuvaana na SJ Saou­ra ya Algeria timu ambayo anachezea Mtanzania, Thomas Ulimwengu, wakikutana katika mchezo wa awali wa Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ridhiwani alisema kuwa Simba ipunguze siasa kuelekea mchezo huu kwa kumtaka Manara apunguze kuzun­gumza sana na badala yake asubiri matokeo uwanjani na kuwataka wajiandae ipasavyo kuhakikisha wa­naibuka na ushindi kuele­kea mchezo huo kwa kuwa ndiyo wawakilishi pekee hapa Bongo.

“Nawatakia Simba kila la kheri kuweza kupata ma­tokeo mazuri na kushinda mechi yao ya Jumamosi kwani wao ndiyo wawak­ilishi wetu pekee ambao wamebakia kwa sasa katika michuano ya kimataifa.

“Kwanza kabisa naomba wapunguze siasa kuelekea mchezo huu, Manara ame­kuwa akizungumza sana kupitia mitandao ya kijamii hivyo ni vyema akaacha kuongea sana na badala yake asubiri mechi ichezwe na timu iweze kujiandaa vyema kuelekea katika mchezo huo.

“Jambo lingine am­balo nimependa ku­washauri Simba ni katika suala hili la vi­ingilio ambapo kuna kiingilio cha shilingi laki moja huku wenye magari yao watatakiwa kuacha hotelini, jambo hili si sahihi siyo watu wote wenye kiasi hicho cha fedha cha kuweza kutoa ili kuingia uwanjani.

“Wawaache watu waingie uwanjani wakafurahie mpira kama ilivyokuwa katika michezo iliyopita ikiwemo dhidi ya Nkana ya Zambia watu waliingia wengi na walifurahia, siyo hivyo wa­navyotaka kufanya, utara­tibu kama huo wenzetu Ulaya wanaufanya shabiki ananunua tiketi kwa mwaka mzima.

“Waache kufanya maa­muzi ya kukurupuka, uwanjani siku zote hakuna viti vya VIP na badala yake kuna viti vya watazamaji, walizingatie hilo ili kupata mashabiki wengi wataka­okwenda kuishangilia timu yao,” alisema Ridhiwani.

8 COMMENTS:

  1. Kikwete junior usitafutwe mashaka ya bure kutoka kwa Manara labda asiamue kukulipua mambo ya Simba mwachie Manara hakuna jambo litakalofanikiwa bila ya kufanyiwa majaribio.Ni ndio maana Simba wanatoka Yanga "wanatota" kama Simba wakiweka v.i.p laki moja,laki mbili ni maamuzi yao wenyewe mechi za ubingwa bado zipo mbichi na mechi ya kesho itasema yenyewe kama ada ya laki moja ina tija au la kwa klabu ila tunapaswa kuwapa hongera Simba na sio kuwavunja moyo kwa ubunifu wa aina mabali mbali katika kujitafutia mapato ya ziada kwa maendeleo ya klabu yao. Nguvu ya kujaribu jambo kwa nia njema ni bora zaidi hata kama utafeli kuliko kutofanya kabisa. Ni vizuri Ridhwani akapambana na wanaoihujumu Yanga kuliko kutafuta kiki kwa Manara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaan maelezo mengi nkajua yana point kumbe mapovu tuu

      Delete
  2. Ridhiwani ana akili aizungumzie yanga sio simba yetu mama wewe siasa nini mbona umwambii disms teni aache siasa ya kuzungumzia ndani ya chumba na laptop tutaacha kuwachangia nauli mshindwe kusafiri tena wewe na mpira ni wapi na wapi ulikuwa unachezaga rede kwaio acha vizazi vya soka vizungumzie soka wewe zungumzia wizi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbna povu tu shida nn ukwel unauma ee

      Delete
    2. Sasa wenye povu ni vyura tu kama nyny, kwanza mmenunua mawigi muwe waarabu maana jezi mnazo

      Delete
  3. Manara kaajiliwa kwa kazi ya USEMAJI "Ndiye msemaji wa klabu ya Simba". Asiposema Manara unataka nani aseme? au unataka aje Ten ndiye aseme? Kazi ya Uhamasishaji ndio kazi ya Manara, hakuna mwingine wa kufanya kazi hiyo ndani ya klabu. Ridhiwani, fanya kazi zingine kama hiyo uliyoisemea kuwa "unawatakia simba ushindi", hayo mengine tuachie Simba yetu. kuhusu viingilio huo ndio ubunifu tunaoutaka, hatutaki kuwaiga ulaya hao wanaouza tiketi mwaka mzima. Sisi tunauza kwa muda huo uliotolewa, mwenye laki atyanunua asiye nayo atanunua za elfu 10 na za elfu 5. Na zaidi ya hapo hakuna atakayekamatwa na polisi kulazimishwa kununua tiketi za laki moja, ni hiari ya mtu.

    ReplyDelete
  4. Manara anawatia moyo wanasimba....na Kazi hii inafaa kufanyika kabla ya mchezo.... Sasa Ridhiwani unataka maandalizi baada ya tukio??😨😨😨...unakosa sifa nzuri kuwa kiongozi

    ReplyDelete
  5. Tena tiketiza laki 1 ni 300 tu.Ni ubunifu mzuri. It is better to try and fail than not to try at all.
    Kuna timu yake haina hata nauli haisemei kazi kuropoka kuhusu Simba.
    Manara anafanya kazi nzuri sana Simba nä waliompa kazi hiyo ndio wanaelewa.
    Yeye huyo anayekereka hawezi hata kuujaza uwanja wa watu elfu 10!
    Siasa zipi alizofanya Manara?
    Mtu yupo uchi anazungumzia mtu aliyevaa suti bila tai.
    Vaa nguo kwanza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic