December 9, 2019


Baada ya kuamua kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu ya Yanga, mshambuliaji Sadney Urikhob amesema viongozi wengi wa timu hiyo ni wababishaji. Imeelezwa.

Taarifa imesema kuwa Urikhob amekuwa akiwaulizia mara kwa mara juu ya malipo yake na wao wamekuwa wamekuwa wakimpiga kalenda kila siku.

Imeeleza kwa kusema kuwa kila mara mchezaji huyo alipokuwa akikikumbushia kulipwa fedha hizo viongozi wamekuwa si wakweli na ikabidi mpaka afanye maamuzi hayo.

Urikhob ambaye hivi sasa yuko kwao Namibia, amesema mabosi wake wamekuwa wakisema hawana fedha na badala yake wamekuwa wakimweleza aendelee kuwa na subira.

6 COMMENTS:

  1. Hatari,Tulishawahi kuwapa ushauri Yanga kwamba Simba ilipokuwa vibaya huko nyuma haikushindana na Yanga ya yussufu Manji katika usajili wa wachezaji. Simba iliamua kulea na kukuza wachezaji wake wenywewe vijana na licha ya kutokuwa na wachezaji wa kigeni Simba hiyo iliisumbua Yanga iliyosheheni wachezaji mahiri wa kigeni. Yanga haiwezi kushindana na Simba hivi sasa kiuchumi waisitaabike.Viongozi wao wanatakiwa kutumia akili zaidi kukabiliana na simba kuliko nguvu ili kuepuka aibu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio unaiogopa Simba sio yanga usituletee ushamba wako hapa Simba ni ya kawaida sana

      Delete
    2. Unaambiwa ukweli unatoa mapovu.Mbaya zaidi wachezaji wa kigeni wanadai na yote nikutaka kushindana na Simba.Tuliwasajili usiku usiku kwa mbwembwe na viwango vyao duni.Ni bora tungetafuta wach zaji kama kina Ngasa waliomua kucheza kwa usajili wa bure.Ukweli usiopingika tusipobadilika na kubaki na longolongo zetu basi kwa mwenendo alio nao Simba itakuwa kama mbingu na ardhi.

      Delete
    3. Januari 4 ndio utajua kuwa Simba si ya kawaida kama unavyodai. Simba ni level nyingine...

      Delete
  2. Msolla tuachie timu yetu na mbwa wenzio nyie niwezi hamna uwezo wa kuitoa timu hapa ilipo!(gsm)(gesi)(sport pesa)(azam na nk hawatoi pesa?ondokeni nyie niwezi

    ReplyDelete
  3. Na viongoz wa vyura wasipokuw makin tareh 4 kuna m2 anapigwa hamsa pale,,,,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic