Bao pekee la Hassan Abdallah limeipa ushindi Timu ya Taifa ya Kenya kwa kufunga Kilimanjaro Stars 1-0 kwenye mchezo wa CECAFA uliofanyika Uganda.
Katika mechi hiyo ya kwanza imeonekana kuwa nzuri kwa Kenya kwa kucheza kandanda safi huku ikitawala zaidi.
Kipa wa Stars Aishi Manula alikutana na mtihani mzito kufuatia kukutana na makombora kadhaa kutoka kwa wapinzani wake na akiokoa michomo mingi.
Kibarua kingine kwa Stars kitakuwa dhidi ya Zambia Jumanne ya wiki ijayo.








0 COMMENTS:
Post a Comment