December 9, 2019


BRUNO Tarimo maarufu kama ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa amesema kuwa siri kubwa ya kupata ushindi mbele ya bondia Nathaniel May raia wa Australia ni kujituma bila kukata tamaa.
Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kg 59 lilifanyika Ijumaa nchini Sydney  lilikuwa ni la kuwania mkanda wa International Super Featherweight Defense (IBF) ambao ameutwaa Vifuaviwili baada ya kushinda kwa pointi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Vifuaviwili alisema kuwa alijipanga kupeperusha bendera ya Tanzania akiwa ugenini jambo ambalo lilifanikiwa kujibu kwa kupata ushindi.
“Haikuwa kazi rahisi kwani pambano lilikuwa gumu na kwa kila aliyeona ataamini, ujue sio kazi nyepesi kushinda tena kwa pointi ugenini ni jambo gumu sasa kikubwa ni juhudi na azma yangu ya kupeperusha bendera ya Tanzania imekamilika,” alisema.
Vifuaviwili ameweka rekodi tamu kwa Tanzania kwa upande wa ngumi kimataifa akicheza jumla ya mapambano 28 amepoteza pambano moja kwa pointi na akishinda jumla ya mapambano 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic