December 15, 2019


Mwenyekiti wa timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga Herison Maeja, ametangaza kijiuzulu nafasi hiyo, kwa madai ya kuzidiwa na majukumu.

Maeja ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kuwa ifikapo Decemba 15 mwaka huu, hata kuwa tena mwenyekiti wa timu hiyo ya Stand United.

Amesema kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kazi zake binafsi, hivyo hatakuwa na uwezo wa kuisimamia timu hiyo tena kwa ufanisi, hivyo ni vyema akawaachia watu wengine waiendeleze, ili ipate kutoa burudani kwa wapenzi wake pamoja na kupanda tena daraja na kushiriki ligi kuu.

“Kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kazi zangu, hivyo sitakuwa na nafasi mwafaka wa kupambana na kutekeleza majukumu magumu na mazito ya clabu kwa ufanisi, hivyo kwa heshima na taadhima ninaomba kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa clabu ya Stand United FC ifikapo Decemba 15 mwaka huu,”amesema Maeja.

“Kwa unyenyekevu mkubwa shukrani zituendee sisi sote pale timu yetu ilipofanya vizuri na kuleta sifa kwa wana Shinyanga kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, wanachama, wapenzi, na wadau mbalimbali, jina la Mungu lipewe sifa, lakini pale ambapo timu haikufanya vizuri changamoto kubwa ilikuwa ni ukosefu wa fedha.

“Mishahara kwa wachezaji ilikuwa haitoshelezi, ukosefu wa fedha za usajili wachezaji bora, ukosefu wa posho za safari, na uhaba wa vifaa, lakini nitaendelea kuwa mwanachama na nitashirikiana na uongozi utakao kuwepo bega kwa bega ili kuirudisha timu yetu kushiriki ligi kuu tena,”ameeleza Maeja.

Aidha Maeja alijiunga na timu ya Stand United kama mwanachama wa kawaida mwaka (2013), na (2015) alikuwa mjumbe wa kamati kuu, na mwaka 2016 alichanguliwa kuwa mwenyekiti wa timu hiyo, ambapo katika msimu uliopita wa ligi kuu timu hiyo ilishuka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic