December 26, 2019


UONGOZI wa Klabu ya Nkana ya nchini Zambia, umeweka wazi kuwa hawajavunja mkataba na beki wao, Mtanzania, Hassan Kessy kama inavyoelezwa kuwa ameachana na timu hiyo.

Juzi mchana kuliiibuka taarifa za beki huyo kuwa ameachwa na timu hiyo kwa kuwa hakuwepo katika mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo dhidi ya Power Dynamo uliopigwa kwenye Uwanja Arthur Davies uliopo Kitwe nchini humo huku Nkana ikipoteza kwa kipigo cha mabao 3-0.

Championi lilimtafuta Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Charles Chakatazya, alisema kuwa Nkana haijavunja mkataba na beki huyo kama inavyoelezwa kwani hakuwepo kwa muda kutokana na matatizo ya kifamilia.

“Kessy wala hatujavunja naye mkataba kama inavyoelezwa na siyo kweli bado ni mchezaji wetu kutokana na mkataba uliopo.

“Lakini hakuwepo kwa sababu ya matatizo ya kifamilia, alienda Tanzania kumuuguza baba yake mzazi anayeishi Morogoro ambaye alikuwa mgonjwa ila tunavyoongea ameshafika Kitwe kuungana na timu, hatujavunja mkataba wala yeye hakutaka kuvunja mkataba, bado tuna mipango naye mirefu,” alisema Chakatazya.

1 COMMENTS:

  1. Ushauri
    Tafadhali unaposoma ujumbe uupeleke aidha kwa njia ya simu/email/mdomo Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuhusu mchezo uliopangwa kufanyika uwanja wa sokoine Mbeya Ijumaa tarehe 27 mwezi wa 12, uhamishwe upelekwe iringa katika uwanja wa samora....kwakuwa uwanja wa sokoine umeharibiwa vibaya mno na tamasha la sanaa lililofanyika jana likiwahusisha WCB Rayvanny na Diamond, mpaka sasa hivi tunapozungumza...haufai kwa matumizi ya mchezo wa soka, na ni hatarishi kwa afya za wachezaji

    Ahsante

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic