December 7, 2019


UWANJA wa Ad Diriyah, mjini Saud Arabia majira ya saa 1:00 usiku kutakuwa na pambano la kukata na shoka kati ya Antony Joshua na Andy Ruiz Jr watachapana makonde yenye ujazo.

Pambano hilo ni la uzito wa juu ni la marudiano na mabondia hao watakuwa wanawania mikanda ya WBF, IBF na WBO ambayo yote kwa sasa ipo mikononi mwa Ruiz Jr ambaye alimdunda Joshua raundi ya saba katika pambano la awali lililochapwa Juni Mosi mwaka huu.

Joshua anashika namba tatu duniani kwa ubora kwa mabondia wa uzito wa juu ameanza kupambana tangu 2013 amepoteza pambano moja tu kwenye rekodi zake mbele ya Ruiz Jr na ametamba kuwa leo atalipa kisasi jumla.

Ruiz Jr amesema kuwa anatambua mapigo ya Joshua hivyo hana mashaka lazima atamdunda tena bila kuhofia lolote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic