December 27, 2019


Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kutuma barua kwenda Bodi ya Ligi ya Tanzania (TPLB) ili kurejeshewa gharama walizozitumia kuelekea mechi yao na Tanzania Prisons.

Taarifa zinasema kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, ameeleza wamekuwa wakitumia fedha nyingi wanaposafiri kwenda ugenini.

Maamuzi ya Yanga kutaka kufanya hivyo ni kutokana na bodi hiyo kubadilisha uwanja wa kuchezea kutoka Sokoine Mbeya ambao umehabribiwa na tamasha la muziki lililofanyika juzi kwenda Samora Iringa.

Kutokana na mabadiliko hayo, Yanga wameeleza kuwa utawaingiza kwenye hasara lakini akisema pia watapambana kugharamika sababu wanapigania ubingwa.


4 COMMENTS:

  1. Sababu za kubadili kiwanja si zimetolewa kuwa kimeharibika na Hakuna jengine isipokuwa kuhamia kwengine na isijekuwa kisingizio tosha ikiwa Yanga itashindwa kutamba hasa kutokana na vitisho vya kocha wa Prison

    ReplyDelete
  2. Jamaa wanajichanganya Sana. Inafaa watulie na kujipanga

    ReplyDelete
  3. Ni ukweli bora watulie na wasubiri kipigo toka kwa mnyama

    ReplyDelete
  4. Nyie inaonekana ni wapuuzi msiojua hata taratibu na sheria za soka letu.......iko wazi kuwa endepo chama cha soka kitabadilisha uwanja uliotakiwa kutumiwa awali kutoka sehemu moja kwenda nyingine au kuahirisha mechi wakati timu moja ilishaingia gharama za safari,chama cha soka kinapaswa kufidia hasara itakayojitokeza na ndio maana yanga wamesema hivyo kwakuwa wanajua taratibu na sheria sio kama nyie mnaokurupuka tu na kuongea msichokijua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic