December 10, 2019


Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Yanga imesema kuwa wapo tayari wawaachie wachezaji wao wote wa kimataifa waondoke lakini siyo mshambuliaji Mkongomani, David Molinga na Mghana, Lamine Moro.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu wapate taarifa za wachezaji wao sita wa kimataifa kutangaza kuvunja mikataba yao na kujipanga kurudi nyumbani kwao kwa kile kilichotajwa madai ya malipo ya mishahara ya miezi miwili.

Wachezaji hao ni Issa Bigirimana, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Sadney Urikhob, Molinga na Lamine ambao wote walisajiliwa kwenye msimu huu wa ligi.

Kwa muijibu wa kikao kilichokaa jana cha Kamati ya Ufundi na Mashindano ya timu hiyo, kwa pamoja wameridhia wachezaji hao kuondoka huku wakiweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakisha Molinga na Lamine kwa kuwalipa madai yao ili warejee kikosini.

Mtoa taarifa huyo alisema wachezaji hao wengine wanawaachia kutokana na kutokuwa na mchango katika michezo ya Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa waliyokuwa wanashiriki.

Aliongeza kuwa tayari uongozi umeanza kufanya jitihada hizo za kuwarejesha kikosini nyota hao wawili licha ya kuandika barua za kusitisha mikataba yao.

“Ni ngumu kwa viongozi, pia kaimu kocha wetu Mkwasa (Charles) kukubali kumuachia Molinga na Lamine kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwenye timu katika michezo ya ligi.

“Hivyo viongozi wamekutana leo (jana) haraka kwa ajili ya kukamilisha mipango hiyo ya kuwarejesha kikosini wachezaji hao kwa kuwalipa stahiki zao za mishahara na posho wanazodai.

“Tunafahamu umuhimu mkubwa wa wachezaji hao wawili tukielekea kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba, hivyo ni lazima warejee kikosini, lakini hao wengine tupo tayari kumalizana nao kwa kuwaacha waondoke zao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo alisema: “Hilo suala lipo kwenye Kamati ya Utendaji na siyo kwangu, hivyo likifika kwangu nitalizungumzia.”

3 COMMENTS:

  1. Yanga yanga yanga yanga enyi viongozi mnadhani mtaendesha timu kiujanja janja mpaka lini? wao kuandika barua ya kuvunja mkataba sio kwamba hamtawalipa stahiki zao hapana, maana wao wamefata sheria kabisa usipo mlipa mtumishi wako ndani ya miezi mitatu basi umevunja mkataba na yeye lakini lazima umlipe stahiki zake zote za nyuma sasa kweli kama ni kweli kulingana na taarifa hii bas viongozi wanataka wapitie kwenye kivuli kuwa wao ndo wamevunja je, umewalipa chao chote? msikimilie kusajili tena ebu fumbeni macho msawazishe haya makovu kwanza, maana hata hapa nyumban wakina moro wapo wengi sana. mambo yakiwa sawa basi mtasajili jaman msijilinganishe wenzetu tayari wametuacha Ninyi viongozi mtuonee huruma tuanumia mioyo inasononeka. Wengne walikuja pale tshirt za Yanga zinawatosha kabisa sasa hv Kama mwakalebela havai jezi hata kidogo maana tumbo nyumba, mwingne ndo usiseme nyie mpigeni lakin Siku yenu inawadia tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh balaa hili eti wengine tumbo nyumba.Hata miezi Sita haijaisha mambo yameshaharibika ndani ya Yanga.

      Delete
  2. Mimi siafiki uamuzi uliochukuliwa na Kamati Tendaji ya kuachana na wachezaji wa kigeni. Wana makosa gani. Mtu kudai chake ni kosa. Pili kuna mechi mbele yetu na Simba. Mechi hii inahitaji maandalizi na tayari wachezaji hawa walikwishafahamiana kisoka. Uamuzi wa kuachana nao naona siyo wa busara na unatakiwe ufikiriwe upya. Tunataka mechi kati ya Simba na Yanga ndo ipate ushindi na wachezaji hawa wa kigeni wakiwa wameshiriki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic