December 12, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umeamua rasmi kuvunja mkataba na mchezaji, mshambuliaji Juma Balinya kutoa Uganda.

Maamuzi hayo yamekuja kufuatia makubaliano ya pande zote mbili juu ya kuvunja mkataba huo.

Licha ya makubaliano hayo, taarifa za ndani zinaeleza Balinya alidhamiria kuondoka mwenyewe Yanga kutokana na kutolipwa fedha zake za mshahara kwa muda wa miezi mitatu.

Mbali na Balinya, wachezaji wengine ambao wanatajwa kuondoka ni David Molinga, Sadney Urikhob ambaye tayari ameshasepa muda na Sadney Urikhob.

2 COMMENTS:

  1. Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
    Unajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup

    Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji
    1. Sadney Urikhob
    2. Juma Balinya
    3. Maybin Kalengo
    Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
    Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikawa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
    Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa. Nadhani Simba Sports Club inaendeshwa kisayansi na kisasa zaidi na CEO mpya kuliko Yanga....wao wanaendesha kwa kisiasa na kiswahili!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa kama pesa namna na madeni mengi wafanyaje wao??

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic