January 17, 2020


Aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa hajui hatima yake ndani ya klabu hiyo mara baada ya ujio wa kocha mpya Mbelgiji, Luc Eymael.

Yanga imemleta Eymael kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambapo Mkwasa alikuwa akikaimu kwa muda tangu kutimuliwa kwa Zahera mwishoni mwa mwaka jana.

Mkwasa amesema kuwa, kwa sasa bado hajui hatima yake ndani ya kikosi hicho baada ya kocha mpya licha ya kuendelea kuwepo kikosini, huku akisema hafahamu kama atabaki au la.

“Tumefurahi ujio wa kocha mpya ndani ya Yanga na tutatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anafanya kazi vizuri kwa kumuelekeza utaratibu wote wa timu.

“Kwa upande wangu bado sijajua hatma yangu viongozi ndiyo wanaojua na ndiyo wenye majibu kuhusu uwepo wangu ndani ya timu, kwa sasa bado naendelea kukinoa kikosi hadi kocha mpya atakapotambulishwa rasmi kwani kwa sasa bado hajakabidhiwa kikosi,” alisema Mkwasa

2 COMMENTS:

  1. Hatutaki kusemamengi lakini tumeona tafauti juu ya uliyoyafanya wewe na anayoyafanya mzungu na juu ya hivo huna hakika juu ya kubakia kwako. Usitaraji kushukuriwa na ujiweke tayari, ndio tulivo

    ReplyDelete
  2. Yeye(Mkwasa) inafahamika kuwa alikuwa anakaimu, sasa inamaana mpaka Leo hii MTU hajui nini maana y kukaimu? Au maana yke kuwa ukikaimu basi ndio upewe mkataba wa kudumu? Najua Master no kocha mzuri pia mzoefu na ni full Yanga lkn isiondoe maana ya kukaimu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic