January 22, 2020


Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, ametaja kwamba kucheza kwa haraka na kutumia mfumo wa 4-3-3 ndiyo silaha pekee ambayo inamfanya ang’ae na kupata matokeo mazuri hadi sasa.

Mbelgiji huyo katika mechi zake tano za ligi alizoisimamia Simba, ameshinda mechi nne na kukusanya pointi 12 huku akipata sare mechi moja tu na Yanga.

Sven akiwa kocha wa Simba alishinda mbele ya Lipuli FC mabao 4-0, KMC 2-0, Ndanda 2-0 na Mbao FC 2-1.

Mbelgiji huyo ameliambia ChampionI Jumatatu kuwa aina ya mbinu yake hiyo ndiyo ambayo imekuwa ikiwazidi wapinzani wake wengi na kushinda mbele yao kila anapokutana nao.

“Mfumo wangu ni 4-3-3 ambao ndiyo nautumia kila mechi, mara zote nacheza kwa mfumo huo na ndiyo umetupa ushindi hadi sasa.

“Tukicheza hivyo inatufanya tunakuwa na kasi sana na tunacheza kwa haraka zaidi ya wengine, jambo ambalo ndiyo linatufanya hadi sasa kushinda mechi zetu hizi ambazo nimesimama hadi sasa.”

3 COMMENTS:

  1. Ni bora ukaficha siri yako isije ikaigwa kama Walivoiga usajili ambao waliufanya na huku macho yakiwa yamefungwa

    ReplyDelete
  2. siri gani wakati style ya 4-3-3 inajulikana dunia nzima na kila shabiki wa mpira

    ReplyDelete
  3. Msibishane sana kwa yanayoandikwa humu, sio ya kuaminika sana, juzi tu the same blog iliandika Sven anasema hataacha falsafa yake ya kucheza na mshambuliaji mmoja, leo mfumo wake ni 4-3-3!
    Hii blog si ya kuiamini sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic