January 22, 2020


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na diwani wa kata ya Mwanga kaskazini Baba Levo amefunguka na kuonyeshwa kukerwa na baadhi ya vitu vilivyotokea mkoani Kigoma katika show ya Diamond ya kuazimisha miaka 10 yake kwenye tasnia.

Baba Levo ameonyeshwa kukerwa na Diamond huku akisema; “Diamond alifanya makosa mawili makubwa na sisi huwa ni wasema kweli pale linapotokea jamboi, tatizo la kwanza ni kwa baadhi ya wasanii kutopanda jukwaani na kufanya show na hiyo ndio ilipelekea fujo nyingi mpaka watu wakaanza kurusha mawe.

“Tatizo la pili ni kujenga msikiti na madrasa kwani aliangalia kwa upande wa waislamu tu, hilo amefanya Udini, basi angejenga Kanisa ili kuleta usawa, mimi nilimshauri ajenge soko maana kuna akina mama kama mia nne hivi wanapata shida na hapo wanenda watu wote Wakristo, Waislamu lakini akakataa,” amesema Baba Levo.

6 COMMENTS:

  1. Hahahahaha kwan huoo msikiti kaujenga au kaukarabati tuu
    Vp muheshimiwa diwanii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata kama ameukarabati anatumia mwenyewe au watu wengi wakigoma na sie tusio wakigoma?We Diwani nenda kwa dudu baya muombe akujengee kanisa hapo mwandiga ili upate cha kuongea kwenye kampeni zako

      Delete
  2. huyu diwani ndie mbaguzi maana Tanzania mtu akijenga msikitini ni poa tu na akijenga kanisa pia ni poa tu wala hakuna atakayeulizwa na hata Raisi wetu kasaidia katika kujenga misikiti sasa la ajabu nini hapo

    ReplyDelete
  3. Wewe kama diwani ungeanza kwa kuonesha mfano wa hicho unachokisema,nina hakika kama ingetokea Diamond amejenga bar,night club,danguro au chochote chenye kuwafurahisha wanadamu ungepongeza na kuomba ajenge nyingine

    ReplyDelete
  4. kwa hiyo ww unamgundisha mtu afanye unavyotaka ww mbona kule tandale aligawa bima za afya kwa watu wa pande zote we huoni hilo

    ReplyDelete
  5. Ney wa mitego amejenga kanisa , kuna ubaya gani hapo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic