Kocha wa Simba, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amelalamikia bao la Yanga akidai kuwa lilifungwa wakati mchezaji wake akipatiwa matibabu nje ya uwanja.
Alisema kuwa wakati mchezaji huyo akiomba kuingia uwanjani, mwamuzi hakumuona na goli likafungwa. Hatahivyo hakutoa lawama kwa mwamuzi Jonesia kwani alisema dakika zote alikuwa sahihi.
“Siwezi kumlaumu mwamuzi lakini tulifungwa bao wakati mchezaji wetu akiwa nje ya uwanja bila mwamuzi kufanya uamuzi wowote, “alisema Vandenbroeck.
Naye kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema mchezo huo ulikuwa mgumu, hasa pale walipokuwa nyuma kwa mabao mawili, “lakini mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani wa hali ya juu. Alisema kuwa walipania kushinda mchezo huo, lakini walitarajia matokeo hayo.
“Mtokeo tuliyatarajia wachezaji walikuwa vizuri, licha ya kwamba tulitaka matokeo yaushindi katika mchezo huo, “alisema Mkwasa.
Alisema baadhi ya wachezaji ambao hawakupewa nafasi katika mchezo huo atawatumia katika mechi zijazo ili kuhakikisha anatengeneza timu bora zaidi na yenye ushindani katika mbio za kuwania ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment