January 5, 2020


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa wanawekeza nguvu kubwa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi litakalofanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Januari 6,2020.
Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 na ina pointi 26 kibindoni mchezo wake wa kwanza ndani ya mwaka mpya 2020 ilishinda mabao 2-1 mbele ya Singida United.
Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa hesabu za kwenye ligi zinafungwa kwa sasa na nguvu zote zinaelekea kwenye kombe la Mapinduzi.
“Sisi ni mabingwa watetezi tunaamini kwamba kazi kubwa kwa msimu huu ipo kwenye kulitetea taji letu ukizingatia kwamba timu zinazoshiriki ni bora nasi lazima tupambane kutetea taji letu,” alisema Cheche.
Azam FC  ipo kundi A ambalo litakuwa Unguja lenye timu za Mlandege, Yanga na Jamhuri itafungua ukurasa wake wa kutetea taji hilo kwa kucheza na Mlandege.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic