January 20, 2020


DEAN Smith, Kocha Mkuu wa Aston Villa amesema kuwa timu yake ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la kuipata saini ya mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta.

Samatta anayekipiga Genk ameifungia timu yake jumla ya mabao 43 kwenye mechi 98 alizocheza akiwa na mabingwa hao watetezi wa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Dean amesema kuwa anakubali uwezo wa Samatta kwa kuwa ni shabiki yake namba moja.

"Tunakaribia kumaliza kila kitu kuhusu kumsajili Samatta, kwa sasa tunakamilisha nyaraka muhimu kuhusu vibali vyake ili apate nafasi ya kucheza kwenye timu yetu.

"Ukweli ni kwamba Samatta ni mchezaji mzuri ana tabia njema na nidhamu tunatumaini tutakuwa naye kwenye kikosi chetu," amesema.

Kwa sasa ishu ya Samatta kilichobaki ni kibali tu ili ajiunge na Aston Villa ambayo inashiriki Ligi Kuu England hii inatokana na sheria zao kuwa ngumu na kali kwa wachezaji ambao ni wageni kuwataka watoke kwenye nchi zilizo ndani ya 10 bora kwenye ubora wa viwango vya Fifa.

 Kwa sasa Samatta anapaswa atumie vigezo vingine ambavyo ni pamoja na thamani yake, timu alizochezea, nafasi yake ndani ya timu ya Taifa na idadi ya mabao aliyofunga kwa kuwa Tanzania ipo nafasi ya 134.

Samatta ambaye alicheza Mbagala Market, African Lyon Simba, TP Mazembe na sasa Genk amekuwa na ngekewa kutokana na juhudi zake na dalili zinaonyesha kuwa kila kitu anacho kwenye mguu wake kwani amecheza mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu kubwa pia ndani ya timu ya Taifa amekuwa na mchango mkubwa jambo linalotoa mwanga kwake kupenya mazima na kila kitu kikiwa sawa leo ama kesho anaweza kutambulishwa rasmi.

2 COMMENTS:

  1. Salehe Jembe acha uongo na kuwalisha watu matango sheria ya ligi ya Uingereza ni ngumu inawataka wachezaji wanaotoka kwenye nchi zilizo si chini ya 100 kwenye kiwango cha FIFA sio kama ulivyoandika kuwa si chini ya 10 ya kiwango cha FIFA.kila kukicha mnaandika makande tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic