EDGER Mtitu aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa timu ya Njombe Mji amebwaga manyanga kwa kile alichoeleza
ni kutokuwa na maelewano na viongozi wenzake ndani ya timu hiyo inayoshiriki
Ligi Daraja la Kwanza.
Njombe Mji ipo
kundi A imecheza mechi 11 inashika
nafasi ya sita ikiwa na pointi 16 kinara ni Dodoma FC yenye pointi 24
kibindoni.
Taarifa zinaeleza kuwa mwenendo
mbovu wa timu hiyo ambayo ilishiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ni moja ya
sababu iliyochangia kujiuzulu kwa kiongozi huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment