January 15, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael na msaidizi wake Riedoh Berdien ambao wamepewa kandarasi ya mkataba wa mwaka mmoja na nusu leo watakuwa na mtihani wao wa kwanza kutesti mitambo yao mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru.
Kagera Sugar iliyo chini ya mzawa, Mecky Maxime mwaka 2020 ipo nafasi ya nane na imjikusanyia pointi 24 itakutana na Yanga iliyo nafasi ya saba na imejikusanyia pointi 25.
Yanga iliyokuwa chini ya Charlse Mkwasa imecheza mechi moja tu mwaka huu 2020 ilikuwa mbele ya Simba na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 uwanja wa Taifa, huku Kagera Sugar ikiwa imecheza jumla mechi mbili na imepoteza pointi sita ilifungwa bao 1-0 na Coatal Union pia ilifungwa mabao 2-1 na Polisi Tanzania.
Luc amesema kuwa mpango wake mkubwa ni kuona timu inapata matokeo mazuri kwenye mechi zake zote atakazocheza ikiwa ni pamoja nah ii ya leo dhidi ya Kagera Sugar huku kwa upande wa Maxime amesema kuwa anawatambua Yanga lazima apambane kupata pointi tatu muhimu.

5 COMMENTS:

  1. Kagera sugars ni vibonde asilia wa Yanga na kocha wa Yanga sio kwenda kutesti mitambo bali ni kwenda kukinyaga kibonde chake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. we shabiki maandazi.....ikitokea kagera wakashinda utasemaje?

      Delete
  2. Ila huu wakati muafaka kwa Mecky Maxim kocha wa Kagera kuwaonesha kuwa wamefanya au wanafanya makosa kuacha kumpa ajira ya ukocha ndani ya Yanga.

    ReplyDelete
  3. koccha sisi mashabiki tunataka ushindi tena si was Gori Moja tunataka magori mengi

    ReplyDelete
  4. Maombi yako yamekubaliwa ulitaka ushindi wa goli nyingi au sio?Tatu nyingi.Kama sio refa zingekuwa J4 kama jina lako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic