January 15, 2020


MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2020 safari yake ilihitimishwa rasmi, Januari 13, Jumatatu wiki hii ambapo mchezo wa fainali ulipigwa kati ya Simba na Mtibwa huko Visiwani Zanzibar.
 Katika fainali hiyo, Mtibwa Sugar iliyo chini ya kocha, Zuberi Katwila ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Simba bao 1-0 kwenye mchezo huo.
 Hakika  ubora wa Mtibwa ulionekana tangu mwanzo kwani  mchezo wa kwanza tu dhidi ya wenyeji Chipukizi ilifanya kweli kwa kuibuka na ushindi kisha kwenda hatua iliyofuata ya nusu fainali ilipoitoa Yanga.
 Mtibwa ambayo imeonyesha kwamba kuna hazina kubwa ya vipaji ndani ya Tanzania iwapo watatumika ipasavyo kwani hakuna mchezaji mgeni kwao anayeitumikia timu hiyo.
 Haikuwa hairahisi kwao kufika hapo ila kujiamini na kujituma  uwanjani ndiyo kumewafanya wakaondoka na ubingwa kwenye michuano hiyo.
 Kocha Katwila alifanya kazi ya ziada na hata kuwaamini vijana wake ambao walifanya kile walichoangizwa na mwalimu wao pamoja na kutumia uwezo wao binafsi.
  Hongera Mtibwa Sugar kwa kutwaa kombe hili kwa mara ya pili baada ya kupita miaka mingi hakika wengine watajifunza kupitia ninyi kwenye michuano ijayo.
  Hivyo ni vizuri kwa zile timu ambazo zinapata nafasi ya kushiriki michuano ya Mapinduzi kujituma  kwa bidii kwa kuhakikisha wanafanya kweli na sio kwenda tu, Mtibwa imetoa somo, hongera Mtibwa Sugar.

1 COMMENTS:

  1. Hamna lolote hapo kukamia mechi ya simba peke ndio kitu kinacholiangusha soka letu lisifike popote. Sioni cha maana chochote kwa mtibwa kujitutumua zidi ya Simba pekee halafu wanaishia kuwa timu ya kawaida mbele ya timu nyengine ndani ya ligi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic