Uongozi wa Azam FC umesema kuwa umejipanga kwa ajili ya kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kuanza Desemba 30 Zanzibar ili kuweza kubeba kombe hilo jumlajumla.
Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema wamefanikiwa kubeba kombe la Mapinduzi mara mbili mfululizo hivyo wakifanikiwa msimu huu litakuwa ni mali yao.
"Tumekubali kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup ambayo yatafanyika Zanzibar tukiwa ni watetezi, tumebeba kombe hilo mara mbili na tunatumaini tutakwenda na kikosi kizima kuchukua kombe hilo liwe la kwetu jumlajumla, tukifanikiwa haritarejea Zanzibar.
"Ushindani ni mkubwa na maandalizi yetu yapo sawa kwa kuwa benchi la ufundi linafanya kazi yake kwa ushirikiano ili kubeba kombe hilo ambalo linaanza Desemba 30 hivyo mashabiki watupe sapoti katika kila hatua," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment