April 16, 2016


MUSTAPHA
Huku Yanga ikijiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly ya Misri, beki wa kati wa timu hiyo, Kelvin Yondani na kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ wamepona majeraha yao na wapo tayari kwa mchezo huo. 

Nyota hao, kwa nyakati tofauti walipata majeraha hayo kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Yondani alipata malengelenge mguuni mwake kutokana na kuvaa viatu vipya na Barthez alipatwa na maumivu ya ghafla kwenye mbavu zake.

Daktari wa Yanga, Edward Bavo, alisema wachezaji hao wote wamepona na wameanza mazoezi ya pamoja na wenzao kujiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly.

Bavo alisema, awali walianza mazoezi mepesi ya peke yao juzi Alhamisi kabla ya jana Ijumaa kujinoa na wenzao ili wawe fiti zaidi.

“Yondani na Barthez wamepona na wameanza mazoezi kwa ajili ya mechi ya Al Ahly tutakayocheza wiki ijayo nchini Misri.


“Tofauti na wachezaji hao, pia nashukuru hakuna majeruhi yeyote kuelekea mechi ya kesho ya Ligi kuu Bara dhidi ya 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV