January 26, 2020


HARUNA Niyonzima, akiwa na Yanga ametumia dakika 327 kupachika bao lake la kwanza na kusema kuwa ni mwanzo wa kazi.

Niyonzima aliyewahi kuichezea pia Simba msimu wa 2018/19 kabla ya kutimia AS Kigali ya Rwanda alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo na kazi yake ya kwanza ilikuwa mbele ya Simba wakati wakilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo wake wa pili ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar na alishuhudia timu yake ikichapwa mabao 3-0 na wa tatu ulikuwa dhidi ya Azam FC wakati Yanga ikifungwa bao 1-0 aliibukia Namfua na kufunga bao lake la kwanza dakika ya 57 baada ya kucheza kwa dakika 326 bila kufunga bao kwenye mechi nne alizocheza.

Niyonzima amesema kuwa kikosi cha Yanga kinaundwa upya kwa sasa na Mbelgiji Luc Eymael ni suala la muda kwa timu hiyo kurejea katika kasi yao na ushindi walioupata mbele ya Singida United umewapa nguvu.

“Kupoteza kwetu mechi zilizopita haina maana kwamba hatujui mpira hapana, tatizo kubwa ilikuwa ni kwenye mfumo wa kocha mpya na wachezaji wengi wageni ila kwa sasa tayari tumeanza kuwa na lugha moja, mambo mazuri yanakuja,” amesema Niyonzima.

Leo Yanga itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic