January 21, 2020


UONGOZI wa Singida United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nswanzurimo umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao wa kesho, Januari 22 dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Namfua, Singida.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata ushindi.

"Tunatambua Yanga ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu ila hilo halitupi mashaka tupo tayari kuona namna gani tutashinda.

"Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwani timu imekuwa ikipita kwenye wakati mgumu ila kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ubora," amesema.

Singida United ipo nafasi ya 16 ina pointi 10 imeshinda mechi mbili pekee katika mechi 16 ilizocheza mpaka sasa.

5 COMMENTS:

  1. Ila ni kweli kupoteza nyumbani mtatengeneza mazingira ya kushuka daraja lazima mshinde mechi za nyumbani

    ReplyDelete
  2. Ila Singida chondechonde nawaomba mtoke sare na Yanga. Maana mkiwafunga hali itakuwa mbaya sana Jangwani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chonde chonde nini wewe, yanga hainunui mechi ila mo na hirizi fc kila mechi mnanunua fungeni midomo

      Delete
  3. Visingizio vya kijinga vimepitwa na wakati .Kagera mliwauzia shillingi ngapi?Azam nae waliwapa shillingi ngapi?Ujinga si umejikwaa wapi bali umeangukia wapi?Yanga wamechanganyikiwa hawajui kinachowasibu.Wamebakia kutafuta visingizio.

    ReplyDelete
  4. ujanja ujanja wakipigwa gsm anasajili bilakushilikisha viongozi wakishinda gsm baba lao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic