January 21, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umesikitishwa na matokeo ya mechi zake mbili zilizopita na kuomba sapoti kwa mashabiki wao.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael lipoteza mechi mbili mfululizo kwa kuchapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC.

Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawajafurahishwa a aina ya matokeo hayo mpaka sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Singida United utakaochwezwa kesho, Namfua.

"Kwa matokeo ambayo tumeyapata tumesikitishwa na matokeo yaliyopita. Mashabiki wa Yanga wanapaswa kutokata tamaa, waendelee kuipa sapoti timu, sasa tunajipanga kumalizana na Singida United kwao,"  amesema Nugaz.

Yanga ipo nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 25 kibindoni.

6 COMMENTS:

  1. SI tulipiga makofi na kuwapa guard of honor wachezaji baada ya kufungwa 3 bila.Sasa tunalalamika nini?Ukipanda bangi huwezi kuvuna mchicha. Matamko kila siku tena ya kupingana .Hassan Bumbuli tumemwacha Molinga Nugaz tupo na Molinga. Haijulikani nani ni nani?Mara kamati zivunje mara zirudishwe.

    ReplyDelete
  2. hayo ndo matokeo yakile tulicho panda!!! haiwexekani ata sikumoja upande njugu mawe uje ety uvune kalanga pengine kama no muujiza lbd

    ReplyDelete
  3. TATIZO KUBWA LA YANGA LIPO TOKANA NA WACHEZAJI KUTOZOEANA NA PIA KUNA TATIZO LA MABEKI WA PEMBENI KUTOANZISHA MASHAMBULIZI NA BEKI 4 NA 5 NI WAZITO SANA NA WANAPOKUA NA MPIRA HAWACHEZI KWA KUUMILIKI MPIRA YAANI BORA LIENDE NA HATA WANAPOOKOA MIPIRA HUA WANAMRUDISHIA ADUI NA COACH ITABIDI ABADILI BEKI AU KUWAFANYISHA MAZOEZI YA CONTROL BALL NA KUA WEPESI ZAIDI - YONDAN UMRI UMEENDA LAZIMA APATIKANE MBADALA WAKE NA TIMU IJIFUNDISHE KUWAPA PRESSURE TIMU PINZANI

    ReplyDelete
  4. Ni suala la muda tu Yanga itarudi ktk form yake, kikubwa kushikamana ktk kila hatua, maranyingi team ikibadili coach na wachezaji kuzoeana inachukua muda.
    Ukiangalia kwa umakini wachezaji wapya na coach mpya lazima kutakua na mkanganyiko

    ReplyDelete
  5. Ama kwa Singida timu inayoshika mkia magoli yasipungue 3 au itakuwa maendelezo ya aibu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic