January 30, 2020


Klabu ya Yanga imesema itamwita mchezaji wake, Ramadhani Kabwili kueleza kwa kina juu ya tuhuma za rushwa alizozitoa dhidi ya Simba hivi karibuni.

Hayo yamesema jana na msemaji wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli katika mkutano wa klabu hiyo na wanahabari jijini Dar es Salaam.

"Alichokuwa anakuongea Ramadhani ni historia na hakuna ubaya kwa mtu kuongelea historia ya malalamiko rasmi yalitolewa kocha wao wa zamani Mwinyi Zahera mwaka jana, hivyo sisi kama klabu tutamuita ili tupate ushahidi wote na tuuwasikishe kwa vyombo husika"

Mapema wiki hii, kipa Kabwili alidai kuwa alifuata na mmoja wa vigogo wa klabu ya Simba na kumwahidi gari aina ya Toyota IST iwapo atakubali kupata kadi moja ya njano ili aukose mchezo kati ya timu yake na klabu hiyo ya Msimbazi.

Hata hivyo, Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka nchini (TFF) imetuma wito wa kuitwa kwa mchezaji huyo ili kupata undani wa sakata hilo huku Simba nayo ikijibu madai hayo na kueleza kufedheheshwa nayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic