TAARIFA za vyombo vya usalama nchini Marekani zinasema kuwa waliofariki mpaka jana katika ajali ya helikopta iliyotokea jana huko Los Angeles, Marekani, ni Kobe Bryant, mwanaye Gianna Maria Onore, rafiki wa mwanaye, Alyssa, ambaye aliambatana na wazazi wake John Altobelli na Keri.
Wengine ni kocha wa Gianna na Alyssa kwenye kituo cha kufundisha mchezo wa mpira wa kikapu cha Kobe anayefahamika kama Christina Mauser, abiria wengine ni Sarah na Payton Chester na rubani Ara Zobayan.
Maelfu ya watu wamefurika nje ya uwanja wa nyumbani wa Los Angeles Lakers, Staples Center muda mfupi baada ya kutokea kwa kifo hicho, kila mmoja akimuenzi Kobe Bryant kwa namna yake.
Katika kituo cha Mamba Sports Academy, wachezaji watoto wote walikuwa wakisubiri kocha wao Christina Mauser, mlezi na kocha wao Kobe Bryant waje na wachezaji wawili ambao ni Gianna na Alyssa kwa ajili ya mchezo uliokuwa unafuata.
Bahati mbaya ni kuwa badala ya kufika wao zikafika taarifa za msiba wa ndugu zao. Hapa walipiga magoti kwa pamoja wakiwaombea ndugu zao hawa wapumzike kwa amani.
Sauti ya mawasiliano ya helikopta iliyoondoka na roho ya Kobe Bryant pamoja na mwanaye na watu wegine saba imenaswa na rubani amesikika akizungumza na waongozaji ndege waliokuwa wanajaribu kuiongoza helikopta hiyo lakini walipoteza mawasiliano kabla ndege hiyo haijapata ajali.
Inaonekana hali ya hewa ilikuwa tatizo kubwa huku kukiwa na uhafifu wa kuona kutokana na kuwepo kw ukungu mkubwa uliokuwa umetanda. Mwongozaji anasikika akimwambia rubani kuwa “upo chini sana” (“You’re too low”).
Haina maana kuwa helikopta ilikuwa inasafari eneo la chini sana, badala yake ni ishara kuwa wakati huo ilikuwa katika uelekeo wake wa kwenda kuanguka hivyo kiongoza mawasiliano hakikuwa na uwezo wa kuielekeza ndege wapi pa kuelekea kwa sababu haikuwa ikiiona kwenye rada.
Mmiliki wa timu ya Dallas, Mavericks Mark, amesema timu yake itastaafisha jezi namba 24 kwa heshima ya Kobe.
Kila mtu ana namna yake ya kuomboleza, Mchezaji wa Atlanta Hawks, Trae Young, ambaye ukiondoa ushabiki, alikuwa mwanafunzi wa Kobe Bryant katika kituo cha gwiji huyo na alibadili jezi yake kutoka namba 11 na kuvaa namba 8 kwenye mchezo wa leo.
Lakini katika kumuenzi Kobe, alikaa na mpira kwenye eneo la timu yake kwa sekunde nane (kisheria unatakiwa kuvusha mpira kwenye nusu ya mpinzani ndani ya sekunde nane) ili kuenzi namba ya kwanza aliyovaa Kobe Bryant ambayo ilikuwa namba 8.
Washington Wizards nao waliamua kupoteza sekunde 24 ikiwa sehemu ya kuomboleza kifo cha Kobe kutokana na Jezi namba 24 aliyokuwa anaivaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment