January 4, 2020


MECHI ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga imemalizika huku timu zote zikitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili.

Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Medie Kagere dakika ya 42 baada kushikiliwa na Kelvin Yondani ndani ya boksi, bao ambalo limedumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Mara tu baada ya Kipindi cha pili kuanza, dakika ya 46 tu Deo Kanda akaiandikia Simba goli la pili, hali ambayo iliwalazimu Yanga kufunguka na kusaka bao kwa udi na uvumba.

Dakika tatu tu baadaye, Mapinduzi Balama akaiandikia Yanga bao la kwanza huku Banka akiiandikia yanga bao la pili na la kusawadhisha kunako dakika 53.

Hadi dakika 90 zinamalizika, Simba 2-2 Yanga.

10 COMMENTS:

  1. Simba iache kelele...bahati yao mikia yenu

    ReplyDelete
  2. Kushangilia droo.Uzembe wa Simba kufanya dharau.

    ReplyDelete
  3. Shangilia sare.Fanya maandamano.

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa SIMBA yafanyieni kazi haya maoni ya mashabiki.. Kiukweli Manula hatufai tena.. Haijui thamani ya Simba kabisa.. Aondoke hata kwa mkopo hana msaada na sisi ndo maana hata Kocha wa timu ya Taifa alimuacha @hajismanara @moodewji @football_senzo @seleman_matola @simbasctanzania

    ReplyDelete
  5. Suala sio drooo, suala droo imepatikana kwa namna gani, Simba wangetulia walikua wanashinda hii gemu...

    ReplyDelete
  6. Acheni mikia..mngeshindia kwenu sio kwa Yanga...mikia kelele mmezidi.. Eti kikosi cha bilioni kinatoa sare na Yanga. Mikia tu nyinyi

    ReplyDelete
  7. MANULA NI MVINYO WA ZAMANI, VIONGOZI KOCHA BENCHI LA UFUNDI TUWE MAKINI NA MANULA LA SIVYO HATA POINTI TUNAZOWAZIDI YANGA TUTAZIPOTEZA

    ReplyDelete
  8. watz sisi sijui tunahitaji nn hasa ?
    huyu manula aliachwa na mgunda mkasema mgundaana bifu na manula au na simba, leo hii mnaona manula hafai ?
    acheni upoyoyo.
    hamtaki kukubali yanga waliingia kucheza nibyi mliingia kuchukua kufunga magoli.
    ndio maana mzamiru kapata joto kwa kaz ya tshimbi na makame, na mna bahati ngasa na kaseke hawakuanza viberenge vile.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic