HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamemuita mlinda mlango wao, Ramadhani Kabwili baada ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kuwa walitaka kumpa rushwa apate kadi ya njano ili asicheze mchezo unaofuata dhidi ya mabingwa hao msimu uliopita.
Kabwili aliongea na kituo kimoja cha radio, jijini Dar es Salaam kuwa viongozi wa Simba walimuahidi kumpa gari aina ya IST kama angepata kadi ya njano ili asiwepo kwenye mechi dhidi yao ingawa mwenyewe alikataa.
Bumbuli amesema hilo ni suala la jinai, wamemuita mchezaji huyo ili kuwapa ushahidii ambao wataupeleka kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua za kisheria.
"Hili ni suala la jinai hivyo tumemuita Kabwili atupe ushahidi ili tupeleke kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki," amesema.
Kijana jinsi alivyo lichukulia hili suala litamtesa. Ni kijana mdogo inaonesha dhahiri yakwamba hana mtu wa muongoza na ni hatari. Katika maisha yake ya kazi hajui wapi ataangukia ila Wacha tuujue ukweli.siasa za Simba na Yanga ni majaribu kwani mchezaji anaweza kujiwa na watu Yanga wakijifanya watu wa Simba kumtest mchezaji kujua ana msimamo gani katika uaminifu dhidi ya timu pinzani.La kushangaza ni kwamba kama angeahidiwa yeye mwenyewe binafsi kuwa akiachia goli atapewa gari ingemake sense. lakini apatishe kadi yeye ili mchezaji mwengine apangwe kwakuwa uwezo wake ni mdogo? Kwa kweli wacha tufuatilie hii ishu na vizuri tukajua mwisho wake bila kuchelewa.Hata hapo hapo kwenye radio kwanini alishindwa kumtaja muhusika au wahusika kwa majina,nini kilimzuia au kawasahau?
ReplyDeleteIt's too late to determine the issue,why now?
ReplyDelete