February 26, 2020


SERGE Gnabry alianza kuitungua Chelsea bao la kwanza dakika ya 51 na aliongeza la pili dakika ya 54 wakati timu ya Bayern ikishinda mabao 3-0 mbele ya Chelsea.

Kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Chelsea walimaliza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Marcos Alonso kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 83.

Licha ya Alonso kuonyeshwa kadi hiyo alishuhudia bao la tatu la ushindi kwa Bayern lilifungwa dakika ya 76 na Robert Lewandowski.

Chelsea inayoshika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England inakibarua cha kupindua meza kibabe Machi 18 ugenini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic