February 27, 2020


RUVU Sooting imetozwa faini ya Tsh 1,000,000.00 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kusababisha kutokea kwa vurugu kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

Imelezwa kuwa mwalimu wa timu Salum Mayanga na wachezaji wa timu hiyo,Shabani Kisiga, Emmanuel Martin na Rajabu Zahiri walikuwa viongozi wa msafara huo Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika Kilimanjaro.


Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni 14(43) ya Ligi Kuu Kuhusu Taratibu za Mchezo.

Pia Ruvu Shooting FC waliomba marejeo (review) juu ya maamuzi yaliyotolewa na Kamati juu ya mchezo wao namba 205 dhidi ya Tanzania Prison FC.

Kwenye mchezo huo Ruvu Shooting ilipoteza mchezo kutokana na kutofata Kanuni ya 14(2l) ya Ligi Kuu kwa kuchelewesha gari ya wagonjwa (Ambulance).

Kamati ilipitia tena shauri hilo na maamuzi kubaki kama yalivyokuwa Ruvu Shooting FC kupoteza mchezo dhidi ya Tanzania Prison FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic