February 12, 2020


LUC Eymael ambaye ni kocha mkuu wa Yanga, ameshangazwa na jinsi mwenendo wa ratiba yao ya ligi ambapo ameweka wazi kwamba hata Ulaya kwenye ligi zenye ushindani mkubwa hawachezi kama wao wanavyocheza.

Kocha huyo amesema kwamba ratiba hiyo inawafanya wacheze mechi kila baada ya siku tatu ambapo ni ngumu kwake kwa sababu wachezaji wake siyo maroboti.

Yanga walicheza Alhamisi iliyopita kisha Jumamosi wakacheza tena na jana Jumanne walicheza na Mbeya City katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Eymael, raia wa Ubelgiji, amesema kuwa wana ratiba ambayo ni ngumu kwao kwa sababu wanacheza mechi zaidi ya tisa katika mwezi mmoja, kitu ambacho ni kigumu kwa sababu wachezaji wake ni binadamu na siyo maroboti.

“Sisi siyo maroboti, ni binadamu, kucheza mechi tisa katika mwezi mmoja siyo kitu chepesi, licha ya kwamba wengi wanaona tunaimarika kila baada ya mechi.

“Huwezi kucheza dakika 90 katika siku tatu tofauti tena katika uwanja wa bandia, hili siyo sawa japokuwa tunatakiwa kucheza kwa sababu ndiyo ratiba yetu, tunaendelea na mbio zetu kwenye ligi.

“Kama ukiwaambia Ulaya wacheze mechi namna hii watalia licha ya kwamba wao wana mazingira bora zaidi hata vyumba vya kuwafanyia masaji wachezaji na vitu vingine lakini hawawezi kufanya hivi. Mechi ijayo nitalazimika kubadili wachezaji kwa sababu ya kuwafanya baadhi yao wapumzike,” alisema Eymael.

4 COMMENTS:

  1. Actually ni tangu mechi ya Mbeya city mbeya na Prison Iringa ndiyo Yanga walikuwa na ratib kama hii.Wamekuwa wakipumzika sana..Simba imekuwa inacheza hiyo ratiba ya wiki hii ya Yanga kwa mechi nyingi sasa..Yanga wamekuwa wanacheza mechi moja kila wiki hata zinapita wiki mbili bila mechi..Hivi kumbe ile ya Mwakalebela kulalamika eti Simba anacheza kila siku wakati wao hawapangiwi ilikuwa unafiki.Walitamani sana Simba icheze jtatu.Tunaomba TFF waipangie Yanga mechi zilizobaki wazikamilishe katika masaa 96! kama itakuwa nje ya Dar basi iwe kila baada ya saa 72.Tunataka bingwa wa haki.kinachotokea Simba kitokee Yanga pia.

    ReplyDelete
  2. mwambieni atulize mshono simba haina vipolwa vingi lakini imecheza mfululizo wao wanamavipolwa ya kutosha wamepumzika kalibia wiki nzima harafu anapiga makelele

    ReplyDelete
  3. Ukimuangalia usoni tu huyu kocha unagundua kuwa ni kilaza

    ReplyDelete
  4. Viporo ni viwili wanaweza kumaliza. Mbona Simba mwaka jana alicheza mechi tatu ndani ya wiki hakulalamika?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic