February 6, 2020

PAUL Nonga, nahodha na mshambuliaji wa Lipuli FC amesema kuwa walizidiwa mbinu kipindi cha kwanza na Yanga jana, Februari 5 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jambo lililowafanya wakapoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Yanga ilipachika mabao yote mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Mapinduzi Balama na Bernard Morrison na lile la Lipuli lilipachikwa kipindi cha pili na David Mwasa kwa mpira wa adhabu uliojaa jumla kimiani.

Nonga amesema:-"Kipindi cha kwanza mbinu yetu ya kucheza ilifeli na kutufanya tushindwe kuzuia mashambulizi ya Yanga, ila mwisho wa siku ni matokeo tunayapokea tutajipanga kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata,".

Lipuli inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 25 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 34 kibindoni.

4 COMMENTS:

  1. pacha kuandika habari nusu nusu sema na alichoongea kapteni..ukiweza weka na video..WAMEZURUMIWA GOLI...kwa maana nyingine wamebebwa!wewe unamnyima mtu goli halafu unamzawadia kona.Kichuya keshawahi funga goli kwa kona..ni magoli mangapi katika kona alizopiga?

    ReplyDelete
  2. Ongea ukweli Jembe wacha kujipendekeza kwa Yanga

    ReplyDelete
  3. Baada ya kuona mbinu za uwanjani watu wamezigundua mmeanza kucheza na vyumba vya kubadilishia nguo vya timu pinzani. Shangaa wachezaji wote hawana nguvu kipindi cha pili. Jamani hili nalo tulifanyie kazi... jmn mnatuulia mpira wetu kisa biashara za wachache.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic