February 3, 2020


Klabu ya Juventus inapanga kutenga paundi za Uingereza milioni 150 wakati wa kipindi cha majira ya joto kumnasa beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 28. (Sun).

Klabu ya FC Barcelona inaelekea kufikia makubaliano ya kumnasa winga wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Chelsea, William mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu. (Marca).

Meneja wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amezuia uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 31 kwenda kujiunga na klabu moja ya nchini Qatar mwezi Januari. (90min).

Meneja wa klabu ya Everton, Carlo Ancelotti ameionya klabu ya FC Barcelona kuwa inapoteza muda wake kwa kujaribu kuwasilisha ofa ya juu zaidi kumnasa mshambuliaji wake wa Kibrazil Richarlison mwenye umri wa miaka 22, wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Star).

Klabu ya Manchester United imeongeza juhudi za kujaribu kumleta kwenye klabu hiyo beki anayekipiga na klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly mwenye umri wa miaka 28. (Mirror).

Beki wa kati raia wa Senegal, Koulibaly huenda akaigharimu Manchester United dau la paundi za Uingereza milioni 90. (Star).

United pia inawania saini ya kiungo wa Leicester City na timu ya taifa ya Uingereza James Maddison mwenye umri wa miaka 23 na pia winga wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 19 wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Standard).

Klabu ya Chelsea inajipanga kuizidi kete klabu yta Manchester United katika kumpata mshambuliaji wa Manchester City, Sancho. (Sun).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic