February 12, 2020


Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa sababu iliyopeleka kushindwa kupata pointi tatu dhidi ya Mbeya City ni kutokana na aina ya mchezo waliocheza wapinzani wao.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa na kulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Mbeya City ikipata bao katika kipindi cha kwanza na Yanga ikisawazisha kipindi cha pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Luc Eymael amesema, "sisi tumecheza vizuri lakini unaona wapinzani wetu walivyocheza, walikuwa wamejaa nyuma na kubakiza mchezaji mmoja mbele".

"Makosa yalifanyika katika kipindi cha kwanza na kupelekea bao tulilojifunga, lakini tulikuwa bora zaidi kipindi cha pili na tukapata bao lakini shida bado ilikuwa namna walivyokuwa wakicheza nyuma", ameongeza.

Mbeya City ipo katika hatari ya kushuka daraja, ikiwa katika nafasi ya 19 na pointi 18 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi 19.

7 COMMENTS:

  1. Basi bora ungewaambia wajipange utakavo wewe ili ushinde

    ReplyDelete
  2. Nasikia tayari Yanga wameshapeleka malalamiko yao bodi ya ligi kuhusu goli la Lamine Moro kuwa halikuwa halali ni offside kwani alibaki yeye na kipa.

    ReplyDelete
  3. mbona wao mwaka jana walipocheza na Simba walipaki basi lakini sikusikia kocha wa Simba akilalamika

    ReplyDelete
  4. Mimi sikuwahi kuisikia Simba hata mara moja ikilalamikia ratiba au kufungwa goli sio la halali ijapokuwa yaliwahi Kutoka magoli kama hayo au mechi za mfululizo kama hizo. Yanga imekuwa na nawazo kuwa wao ndio wanaostahaki ushindi na Hakuna mwengine. na kuzudio kududio la malalamiko Yao ni kujifanya wakali na waogopwe

    ReplyDelete
  5. Wanalalamika kwa kukosa uwezo .Hivyo wanajua wakipiga kelele watabebwa.

    ReplyDelete
  6. Hayo malalamiko bodies ya ligi kuwaeleza kwa mini mbeya city walibaki nyuma na kuacha mchezaji mmoja tu mbele

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic