February 10, 2020

KUELEKEA kwenye mechi ya kesho kati ya Mtibwa Sugar na Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba ametoa kauli ya kishujaa kwa mashabiki na viongozi.

Sven anakumbukumbu ya kupoteza mchezo wake uliopita Uwanja wa Uhuru kwa kuchapwa bao 1-0 na JKT amesema kuwa kesho hakutakuwa na sababu ya kutaja zaidi ya ushindi kwa timu yake.

"Hakuna sababu iwe ni hali ya uwanja, mvua, jua au waamuzi wa mchezo kesho haipaswi kuwa sababu. Ni ushindi pekee ndio tunahitaji na tuna kazi ya kuhakikisha tunafanikisha hilo.”.

Kwenye jumla ya mechi 10 ambazo amekaa benchi akiwa ni Kocha Mkuu baada ya kupokea mikoba ya Patrick Aussems amepoteza mchezo mmoja na kulazimisha sare moja huku akishinda mechi nane za ligi.

3 COMMENTS:

  1. Taifa uwanja mzuri timu unaipanga hovyo tusubiri na huko napo tufungwe tena kwa upumbavu wako unaacha wachezaji tegemeo unawaweka nje unaakili sawa sawa toka tuachie timu yetu kafukuzwa kocha mzuri kaokotwa huyu kaletwa MO anapigwa pesa tu fukuza benchi lote weka watu wapya hao niwale wale tu wanatuuza tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaan kocha huyu kama haelewan na mtola tumekwisha

      Delete
    2. Who is Matola??? Unamaanisha hatuwezi kushinda bila inputs za Matola? Naona watu mnakaririshwa na wachambuzi uchwara.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic