February 4, 2020

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ushindani wa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ni mkubwa jambo ambalo linafanya kila timu kupambana kutafuta matokeo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa kila timu nyingi zinaishi kwenye malengo ambayo zimejiwekea jambo linalofanya ligi izidi kuwa nzuri.

"Ligi kiujumla kwa sasa imechangamka kila timu inaonyesha kile ambacho inastahili kukipata ndani ya uwanja. Timu nyingi zimegunuda siri ya kupata matokeo ni kujituma jambo hili linafanya ligi izidi kukua.

"Kwa upande wetu nasi pia tupo vizuri licha ya kupoteza mbele ya Yanga haina maana kwamba tumeshindwa. Matokeo ya mpira yanatupa mwanga wa kufanya kitu kingine," amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 imecheza jumla ya mechi 18 na imejikusanyia pointi 23 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic