February 4, 2020

SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kuzisaka pointi tatu leo mbele ya Polisi Tanzania.

Simba itamenyana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Taifa saa 1:00 Usiku kwenye mchezo wao wa kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Sven amesema kuwa makosa waliyoyafanya kwenye mchezo wao uliopita mbele ya Coastal Union wameyafanyia kazi jambo litakalowapa nguvu ya kuendelea kupambana.

Kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini amesema kuwa anatambua ushindani ni mkubwa na anacheza na mabingwa watetezi hilo halimpi shida anawaamini wachezaji wake.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 18 na leo zinakamilisha mzunguko wa kwanza rasmi kabla ya kuanza kufukuzia kete za mzunguko wa pili.

Simba mchezo wake uliopita ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union ya Tanga huku Polisi Tanzania ikishinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

3 COMMENTS:

  1. Beki weka nyoni na huyo mbrazil na mbarazil alio funga juzi acheze mbele boko na kagere kama ict imekuja mtupie kichuya na huyo wa msumbiji tuone magoli

    ReplyDelete
  2. bora ungekua wewe ndie coach !! haitoshi mnamuharibia Samatta na sasa mnaingilia upangaji wa wachezaji!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Enter your reply...ahahahhaa Bora uwaambie watanzania wengi tumewaona ili kufuta ujinga tu na siyo kuelimika,mnaojifanya samata ametokea kwenu mtamuharibia mbn tp au genk hatuoni wakipwayuka hovyo, kikubwa tumwombee uzima samata ili apambanie nmba siyo et ananyimwa pasi ishu ilikuwa n kusajiliwa epl na siyo kupewa pasi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic