February 9, 2020


Nguli wa mfumo wa soka la kisasa aliyekuja kufanya kazi na klabu ya Yanga kutoka nchini Ureni, Antonio Domingos Pinto, tayari ameshakutana na viongozi na ataanza mipango ya kuibadilisha klabu hiyo hivi karibuni.

Pinto aliingia nchini wiki iliyopita kwa lengo la kukutana na viongozi jambo ambalo limefanyika kwa mafanikio makubwa.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela, alisema tayari wameshakutana naye na kuzungumza na wamefikia muafaka.

Alisema Pinto yupo tayari kufanya kazi na klabu na majukumu yake yatakuwa yanasimamiwa na kamati ya mabadiliko.

“Alikuja kwa mazungumzo ya awali ikiwemo kuiona Yanga ambayo inahitaji kufanya naye kazi na kumfahamu sasa kinachoendelea ni kuendeleza pale tulipoishia naye ila kila kitu kiimekwenda vizuri,” alisema Mwakalebela

Mtaalamu huyo aliondoka siku kadhaa zilizopita kwenda nchini kwao na atarejea mara baada ya mchakato rasmi kukamilika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic