February 9, 2020


MAURICIO Pochettino, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Spurs anahusishwa kujiunga na Manchester United.

United iliyo chini ya Ole Gunnar Solskjaer imekuwa na mwendo wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu England jambo ambalo haliwafurahishi mashabiki.

Inaelezwa kuwa Pochettino atapewa dili la kuinoa United iwapo kocha wa sasa atashindwa kuimarisha kikosi chake.

Inaaminika kwamba Solksjaer atapigwa chini endapo timu yake itashindwa kumaliza ndani ya sita bora kwenye Ligi Kuu England.

United kwenye msimamo ipo nafasi ya nane imejikusanyia pointi 35 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic