February 25, 2020



SVEN Vandnbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa CCM Kambarage dhidi ya Stand United.

Simba itakaribishwa na Stand United leo majira ya saa 10:00 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora, Kombe la Shirikisho.

Sven amesema:'-" Kila mmoja yupo tayari kwa mchezo lakini kwenye mchezo mmoja hatuwezi kutumia wachezaji wote 29 hivyo lazima kuchagua wachezaji wa kuwatumia.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna tutakavyofanya ili kupata matokeo, imani yangu tutafanya vizuri,".

Simba ilianza hatua ya 62 kwa kuifunga Arusha United mabao 6-0 ikaibukia hatua ya 32 kwa kuifunga mabao 2-1 Mwadui FC na leo inakutana na Stand United hatua ya 16 bora.

3 COMMENTS:

  1. Hakuna cha kuzembea kwani wazungu wanasema..respect is earned not granted..yaani heshima sio kitu cha kupewa tu hivi hivi bali ni kitu kinachotengezwa na mtu mwenyewe binafsi.kwa maana yakwamba Simba wakiingia kwa dharau mbele ya stand United basi aibu itawahusu kwani mechi hizi mara nyingi huwaga hazina heshima tumeona Liverpool kapigwa na katimu cha mchangani.Kama mpenzi wa Simba na kama walivyo mashabiki wengi wa Simba ni matumaini yetu kwa benchi la ufundi kutofanya mzaha kwenye mchezo huu.

    ReplyDelete
  2. Habha ha ha ha mjomba lazima tugawane,au wewe unataka simba achukue makombe yote??haiwezekani brother,i fail to reject your statement concerning liver but you must know,that was a game plan,amin hivyo brother kwani mara ngapi tunaona ulaya kwenye baadhi ya ligi unakuta timu inapanga kikosi cha ajabu?hii ni kwasababu wanazingatia priority zao na sio kila ligi wanaingia kwamba wakashinde hapana.liver angekua anataka kushinda ligi zote anazoshiriki basi ungeona nguvu na morali ambayo angeonyesha,ukishiriki kila ligi kwakujitoa ukumbuke majeruhi pia yatakuandama sana na mwisho wa siku utakosa kote.mfano man united tunaona endapo rashford angalikuwepo kwenye game mpaka leo hii tungekua tunaongea mengine kabisa kuhusu kiatu cha dhahabu msimu huu lakini majeruhi yanamuweka benchi,yuko wapi miraji athumani wa simba kama unakumbuka aliumia wapi?je angekuwepo kikosin mpaka leo nini kingekua kinaendelea?katika kila mchezo kuna kitu wanaita priorities and plans(game plans) so do not argue without knowing the real.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yes, brother umenena vema na ukweli ndo huo nadhan hujaacha neno mashabiki huwa hatujui maana ya kusajili wachezaji 30 na malengo ya timu ni yapi, Malengo ya simba ni ubingwa ukishachukua ubingwa tayari umeenda club bingwa Africa je tena unataka nini FA SI KOMBE LA SHIRIKISHO? Watwambie Madrid na Barcelona walishiriki kombe hilo lakini mwisho wote kombe la mfalme wametoka? kwa sababu malengo yaowote ni ubingwa na unaona wote bado wako kwenye dira. Pia kombe la FA kwa kawaida huwa linahusika na wachezaji wa benchi na kikosi B ndo maana liverpool walibadilisha mpka kocha wakaingia na kocha wa timu B nadhani atakuwa ameelewa sasa. Heshima tuishaitengenza sana mengne haya ni mapito tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic