February 4, 2020


KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema ameanza kuona faida ya mabadiliko ya kikosi kwenye mchezo uliopita baada ya kujaribu kumpatia nafasi kila mchezaji kuonesha uwezo wake kwenye timu.

Sven alitoa kauli hiyo juzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

“Mabadiliko ya kikosi niliyofanya ni kujaribu kumpa kila mchezaji nafasi ya kutoa mchango wake kuna Simba ina wachezaji wengi,” alisema Sven. Katika mchezo huo, alifanya mabadiliko makubwa ya kuwachezesha wachezaji tofauti na waliokuwa wanacheza kwenye michezo mitatu iliyopita hususani dhidi ya Namungo FC walioshinda kwa mabao 3-2.

Awali kabla ya mchezo huo, aliwaahaidi mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuwa atafanya mabadiliko kutokana na kikosi ambacho alikuwa anakiamini kufanya makosa mengi ya kujirudia ambayo yaliyokuwa yanaigharimu timu.

Alisema kikosi kilichocheza mchezo hu, ameona kile alichokuwa anatafuta kwani walikuwa wanacheza kwa kujituma na kuonesha wanahitaji ushindi. Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda alisema kwenye mchezo huo wachezaji wake walifanya makosa ambayo wapinzani wao walitumia kupata ushindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic