February 27, 2020


HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hakukuwa na namna ilikuwa lazima Gwambina FC ifungwe ili kurejesha furaha kwa mashabiki na nguvu kwa wachezaji.

Yanga ilishinda bao 1-0 mbele ya Gwambina FC, jana Februari 26 Uwanja wa Uhuru kweye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora na kutinga hatua ya robo fainali.

Niyonzima amesema:" Tulikuwa hatuna chaguo la kufanya licha ya wapinzani wetu kupambana kutafuta matokeo nasi tulikuwa tunahitaji matokeo kwani hatukuwa na chaguo lingine zaidi ya kupata ushindi ukizingatia kwamba tumetoka kupata sare nne mfululizo." amesema.

Bao hilo la ushindi alifunga Niyonzima dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lilidumu mpaka mwisho wa kipyenga.

5 COMMENTS:

  1. Msijisifu kukishinda kitimu kisichokuwa na jina au sifa nanyi mkitumia kikosi cha mabilioni

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli wee ni nyani usieona kundu lako......hao gwambina tuliochezanao sisi na stand mliechezanao nyie wote wapo daraja la kwanza na uzuri zaidi wote wapo kundi moja ambalo gwambina anaongoza wakati stand ni wa kumi....huyo wa kumi mliecheza nae nyie kawatoa kamasi mpaka kwenye matuta wakati bwana yao anaeongoza ligi tumempiga ndani ya dakika tisini.........sasa hapo we boya kati ya yanga na simba nani anastahili kumcheka mwenzake?.

      Delete
  2. yanga anatumia bilion 1 kakifunga kikosi cha gwambina ndani ya dak 90, simba anatumia bil. 4 amepata ushindi kwa msaada wa penalt baada ya dak. 90 kumalizika bila ushindi.
    gwambina haifahamiki lkn ndio mliokesha mkisema yanga hatoboi kwa gwambina, mkawajaza sapoti na viongoz wenu, sasa aibubi ikawarudia

    kahata,misqyusone,chama,kagere,Wawa,Santos,shibob,kanda, na maproo lukuki lkn STD anawatoa jasho na mna kuja na maneno ya gwambina katimunhakana jina.
    haya ww una jina.
    nenda kaifunge yanga.

    ReplyDelete
  3. Ndio bilioni nne lakini si unaona matokeo. Mmeachwa kwa pointi ngapi na magoli mangapi mmefungwa mechi ngapi na droo ngapi au ndio huna habari na hayo ni matokeo ya bilioni nne ulizozitaja

    ReplyDelete
  4. Basi tufanye mnaongoz ligi wazee wa sare jana ndo mkashona ataimae

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic