February 13, 2020


YANGA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael, raia wa Ubelgiji, Februari 15 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uatakaochezwa majira ya saa 1:00 Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza walipokutana msimu huu kwenye ligi, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Patrick Sibomana Uwanja wa Samora, Iringa. Eymael amesema kuwa utakuwa ni mchezo mgumu ila watapambana kupata ushindi kwani hawana chaguo lingine.

"Kwetu sisi mechi zetu ni ngumu na ushindani ni mkubwa matumaini yetu ni kuona tunashinda ili kuongeza nguvu ya kufika kwenye malengo yetu tuliyojiwekea, hatuna chaguo lingine zaidi ya kutafuta ushindi" amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na poiti 38 baada ya kucheza mechi 19.

5 COMMENTS:

  1. Msiwe na wasiwasi kwakuwa nyie ni mabingwa wa jadi basi hata mkipewa ratiba ya maonevo basi ubingwa ni wenu

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha hakuna povu hapo,mabingwa wa kihistoria a.k.a timu ya wananchi msiwe na shaka wala hakuna namna maana kombe likienda msimbazi kwanza TFF itapata hasara kutafuta kombe jingine na pia itakua kama kuidhalilisha yanga inayobebwa na mhimili wa nchi(serikali),kwa namna yoyote ile lazima kombe lirudi yanga hata kuwapokonya alama itabidi maana hakuna namna.

    ReplyDelete
  3. Kikubwa kazaneni kupaza sauti kwamba SIMBA INABEBWA,ili habari ziwafikie wananchi duniani kote na huyo muhamasishaji mliempata LUCYANA MALYA kocha kila siku alalamika yeye ameonewa kweli ndege wafananao huruka pamoja,shabiki wa yanga mnafanana na kocha wenu,mungu awape sauti kubwa zaidi au waambien waongeze sauti na mimi pia nawasaidia SIMBA INABEBWA TUMECHOKA KUONEWA.

    ReplyDelete
  4. nakuunga mkono kaka wajitahid kupaza sauti tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic