KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wapinzani wao Gwambina walikaza mwanzo mwisho na waliufanya mchezo kuwa wa kukimbizana jambo lililokuwa likiwapa ugumu wa kushindwa kufunga mabao mengi ila mpango wao wa kupata matokeo ulifanikiwa.
Yanga jana iliifungashia virago Gwambina FC kwa ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Haruna Niyonzima aliyetupia bao hilo dakika ya 45 akiwa nje ya 18, Uwanja wa Uhuru.
"Tunashukuru kwa kuwa tumepata ushindi, wapinzani wetu walikuwa na spidi na walifanya mchezo uwe wa kukimbizana mwanzo mwisho uwanjani, ila hilo hatujali tumepata matokeo na hilo lilikuwa lengo letu," amesema.
Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho inasubiri kuchezwa droo ili kutambua wapinzani wao watakaokutana nao kwenye hatua hiyo.
Walitawaliwa mchezo..wakaamua kucheza faulo..na pasi nu za kushitukiza.faulo 25 kwa 11, ball possesion Yanga 49? utafungaje magoli mengi endapo mpinzani wako anatawala game..kama kuna bahati basi lile goli la Niyonzima ni bahati tu.
ReplyDeleteGoli 8 ziliyeyuka vipi Mropokaji mwingine alisema 5.Kucheza uwanjani nä kucheza kwa mdomo ni tofauti KUBWA. Ingekuwa kiwango hicho kimeonyeshwa na timu nyingine KUBWA basi kelele zingekuwa nyingi .
ReplyDeletemkubwa ni mkubwa tu semeni kweli goli la niyonzima ni best goal na anastahili sifa
ReplyDeleteyanga hawakushinda kwa matuta kama mikia
maneno yatawatika sana misukule, isiyojitambua, eti la eti lilikuwa la bahati mbona ww hukufunga la hajira???
ReplyDelete