February 25, 2020

JERRY Muro, aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga wa zamani na sasa ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha amesema kuwa wameshapata pasword ya kuwaondolea mzimu wa sare uliokuwa unaisumbua Yanga hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Muro amesema kuwa sare ambazo wamekuwa wakizipata zimeshapata dawa yake na kazi itaanza kesho mbele ya Gwambina FC Uwanja wa Taifa.

"Hakutakuwa na ugonjwa wa sare tena kwetu tumeshapata pasword ya hizo sare na kesho kazi inaanza rasmi mbele ya Gwambina FC.

"Napenda kuwaambia mashabiki wa Yanga wasikate tamaa kesho wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kuona namna kikosi kitakavyoanza kazi nyumbani, ni mwendo mdundo hakuna sare tena,".

Sare nne ilizopata Yanga ilikuwa ni kwenye mechi za Ligi Kuu Bara mbele ya Mbeya City, Tanzania Prisons, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Yanga itamenyana na Gwambaina majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho utakaochezwa kesho.

2 COMMENTS:

  1. Kesho msiwe na wasiwasi kitimu chenyewe mnachochezanacho ni kidogo na dhaifu

    ReplyDelete
  2. hata Ihefu ilikua ndogo ilipoitoa simba mwaka jana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic