March 23, 2020

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa kuna umuhimu wa kikosi chake kuwa na makali ya kushindana na timu zote Bongo ikiwa ni pamoja na Azam FC, Namungo, Coastal Union na Simba.

Eymael amesema kuwa timu zote ndani ya Ligi Kuu Bara zinaleta ushindani jambo ambalo linamfanya afikirie namna mpya itakayompa matokeo mazuri.

Alipoanza kibarua chake kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 aliambulia kichapo ambapo alianza kufungwa na Kagera Sugar mabao 3-0 kisha akaambulia kichapo kingine cha bao 1-0 mbele ya Azam FC.

Kwa sasa ligi ikiwa imesimama kwa muda, Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 kibindoni baada ya kucheza mechi 27.

"Kuna umuhimu wa kikosi changu kuwa na ushindani na kinatakiwa kiweze kushindana na timu zote za ligi bila kujali nitacheza na timu ipi iwe Kagera Sugar, Lipuli, Mtibwa kikubwa ni kuona tunapata matokeo.

"Viongozi nimewaambia kile ambacho ninakihitaji nao pia wanajua nini ninataka nina amini wakati utafika na timu itakuwa kwenye hali ambayo tunaipenda wote," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic