BEKI wa kati wa Yanga, Said Makapu, amefunguka kuwa amepanga kuondoka kwenye timu hiyo iwapo atapata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa kutokana na kukerwa na vitendo vya kubaguliwa alivyofanyiwa na viongozi wa timu hiyo.
Makapu ambaye amebakisha mkataba wa mwaka ndani ya Yanga, ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mchache tangu aanze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo chini ya Mbelgiji, Luc Eymael licha ya kushindwa kupata nafasi katika kipindi cha nyuma.
Akizungumza na Championi Jumatano, Makapu alisema kuwa licha ya kupata nafasi ya kucheza kwa sasa lakini ndoto yake ni kuona anacheza soka la kulipwa kwa kuwa hakufurahishwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kudai kuwa siyo mchezaji wao.
“Natamani kutoka hata leo kwa sababu yaliyotokea nyuma Yanga, sikuyapenda kiukweli hayakuwa masuala ya pesa ila ni viongozi kutokukubali uwezo wangu, sikupenda, mpaka wakataka kunitoa kwa mkopo.
“Haiwezekani mchezaji kama mimi ukanitoe kwa mkopo hata kama sipati nafasi, unamuangalia kwanza nani mchezaji mwenyewe, unitoe kwa mkopo nikajifunze kitu gani!
“Sasa hivi sipaswi kutolewa kwa mkopo ila niachwe nikacheze sehemu nyingine maana viongozi wa Bongo hawapendi wachezaji, mfano mechi ya Yanga na Kagera ile tunafungwa 3-0 kocha Mzungu (Luc Eymael) ndiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza, akanipanga nianze namba sita ila viongozi wakasema ‘huyu mtu siyo mchezaji wa Yanga’.
0 COMMENTS:
Post a Comment