MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba atachelewa kurejea nchini kufuatia Shirika la Ndege la RwandAir kufuta safari zake zote kwa muda wa siku 30.
Hali hiyo imekuja kutokana na kusambaa kwa Ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Kagere ni kinara wa kutupia akiwa ametupia mabao 19 huku Reliants Lusajo wa Namungo, Paul Nonga wa Lipuli, Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar wakiwa wametupia mabao 11
Taarifa iliyotolewa Jumapili na shirika hilo ilisema kuwa imeamua kufuta safari zake zote kwa muda wa siku 30 kutokana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo kufuatia kuwepo kwa ugonjwa huo.
Kutokana na taarifa iliyotolewa na Wizara Afya ya Rwanda juu ya mlipuko ulioikumba dunia kupitia Ugonjwa wa Covid-19, Shirika la RwandAir linafuta safari zake zote kwa muda wa siku 30 kwa ndege zote.
“Wateja wote waliokuwa wamekata tiketi wana njia nyingi za kufanya ikiwemo kukata tena kwa ajili ya safari za mbeleni na ada ya makato itaondolewa,” ilisema taarifa hiyo.
Kagere kwa sasa yupo Rwanda ambapo amekwenda kwa ajili ya mapumziko amesema kuwa suala la kurejea Bongo litategemea hali itakavyokuwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment