March 16, 2020

YANGA wakati inalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ilikosa huduma ya wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza huku taarifa zikieleza kuwa wamegoma ndani ya klabu hiyo.

Uongozi wa Yanga umesema kuwa hakuna suala hilo ila kuna sababu maalumu ambazo zimewakumba wachezaji wao.

Wachezaji hao ambao walikosekana kwenye mchezo wa jana uliopigwa Machi 15 Uwanja wa Majaliwa ni pamoja na Haruna Niyonzima, Kelvin Yondani, Lamine Moro, Mohamed Issa 'Mo Banka', Adeyum Saleh na David Molinga.

Sababu za nyota hao kuukosa mchezo wa jana zipo namna hii:- Haruna Niyonzima alikuwa na kadi tatu za njano.

 Kelvin Yondani alipewa ruhusa ya Mwalimu kwasababu za kifamilia,David Molinga ambaye yeye aliomba ruhusa kutokana na Mkewe kuwa mgonjwa.

 Lamine Moro, Mohamed Issa (Mo Banka) na Adeyum Saleh. 

7 COMMENTS:

  1. Hao wengine mmeshataja kuwa mna mipango ya kuwatema kwahivo mlitaraji nini. Kila siku eti sababu matatizo ya kifamilia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe unayecommenti hauna hata ushahidi wa unayozungumza kwakuwa unatumiwa unakuja kuleta vitu vya uongo uongo ili kuidhalilisha brand hebu acha maramoja

      Delete
  2. Haya aina ya maadui wengine ni magazeti yanayotumika kuidhoofisha brand kila kona kuna mitego ya maadui wa Yanga

    ReplyDelete
  3. Tusipende kuitetea timu hata kama kuna mambo ya hovyo. Hivi hatujiulizi kwanini haya matatizo yawakute watu sita kwa mara moja? Kipindi ambacho kocha amewakosoa waziwazi baada ya mechi na KMC kuwa wamelewa ushindi wa simba!

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo na kocha aligoma?
    Mchezaji mwenye kadi 3 za njano anakuwa amegoma kivipi?

    ReplyDelete
  5. waBongo kwa porojo, Tupo vzr.
    Fanyeni Mambo yenye faida acheni habari za kuungaunga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic