March 16, 2020

BIGIRIMANA Blaise, mshambuliaji wa Namungo FC amesema kuwa walingia uwanjani wakiwaheshimu Yanga jambo lililowapa hali ya kujiamini na kuweza kugawana nao pointi mojamoja kwa kufungana bao 1-1.

Mabao yote ya jana yalifungwa kwa mtindo wa vichwa ambapo walianza Yanga dakika ya sita kupitia kwa Tariq Seif akimalizia pasi ya Juma Abdul na Namungo walifuata dakika ya 62.

Blaise amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kupata bao mbele ya Yanga kutokana na uimara wa kikosi cha wapinzani wao.

"Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri, tuliingia uwanjani kucheza nao kwa kupambana na kila mchezaji alikuwa na majukumu yake, kwa sasa tunasema asante kwa kuwa tumepata pointi moja sio mbaya," amesema.

Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa imecheza mechi 14 na imepoteza mechi moja ikilazimisha sare nne na imeshinda mechi 9.

4 COMMENTS:

  1. VITENDO VYA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE MAPENZI NA SIMBA

    Mbona watu wa Simba wamekasirika sana mpaka viongozi wa serikali (Waziri Mkuu-Namungo fc & Mkuu wa Mkoa Dsm-Simba&KmC) ambao hawapaswi kuegemea upande wowote wanaipania Yanga (utafikiri Yanga ni timu kutokea Kenya) na wanaonyesha mapenzi yao dhahiri na kwa uwazi hili si jambo zuri na linaweza kuleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii iliyo na umoja uliojengwa na waasisi wa Taifa hili...(Mwl. Nyerere, na Sheikh Karume). Mambo ya Mpira yasitugawe katika umoja wetu na Viongozi waliopewa dhamana ya utawala kwa wananchi....dini zetu, mapenzi yetu kwa timu za mpira yasitugawe!

    sikatai kuhamasisha michezo katika jimbo lake la uchaguzi ila Waziri Mkuu anapotoa kauli yenye amri na maagizo yenye utashi binafsi kwa uongozi wa wilaya kumbuka timu pinzani na waamuzi hufikia kwenye mahoteli na guests zote hizo ziko wilayani kunaweza kukawa na shinikizo la hujuma kufanyika kwenye mchezo husika....hiyo ndiyo hoja yangu. Na pia pale Mkuu wa Mkoa anapoingilia katika kuitunza ahadi ya fedha timu moja iliyo katika Mkoa mmoja na timu pinzani, inaleta taswira ya upendeleo na inajenga imani ya chuki kwa timu nyingine....mapenzi binafsi ya viongozi wa serikali katika timu za mpira nasisitiza kwa mara nyingine yasitugawe na yasitutenganishe kwani huu umoja na mshikamano wa kitaifa na udugu ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu...mwalimu Nyerere na Sheikh Karume na muda mrefu.....(hata wao walikuwa na mapenzi ya timu za soka) lakini hawakuwahi kukandamiza timu nyingine!

    Ni maoni yangu
    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. You people need to stop blaming simba every time when you lose or draw. Making excuses and not taking responsibility it shows how in nature the fans of yanga are. Its pathetic really. Grow up.

    ReplyDelete
  3. Typo, I should have said "in mature "

    ReplyDelete
  4. Most of young african fans are the stupid morons who dont know even to introduce themslves,in a simple identity you will know them by passing through their coments and press speech in youtube.dont mess with them you will be alike.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic